Saturday, August 16, 2014

CELINE DION ASITISHA ZIARA YAKE BARANI ASIA KUTOKANA NA MARADHI YA MUMEWE
Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya nyimbo laini duniani maarufu kama Blues, mwanamama Celine Dion ameamua kusitisha ziara yake ya bara la Asia kutokana na Maradhi ya Mumewe
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 46 amejisogeza karibu zaidi kwa wanadani wake René Angélil (72) anayekabiliwa na maradhi ya Cancer inayomtesa kwa kipindi kirefu sasa
Celine, ameamua kuwa karibu na mumewe zaidi katika kipindi hiki akidai kuwa ni kipindi kigumu na chenye msongo wa mawazo kwake, kutokana na maradhi yanayomsibu mumewe (Rene) kutokana na tumor iliyotolewa kooni mwake Mwezi Disemba, mwaka jana
Amebadilisha tarehe za ziara ya Asia, zinazotarajiwa kuanza Novemba 11 huko Nagoya, Japan. Alipangiwa kuanza ya Las Vegas mnamo Ijumaa hii lakini ameipotezea pia.
“Ninataka kuchangia kila chembe ya nguvu zangu kwa kupona kwa mume wangu, na kufanikisha hilo, ni muhimu kwa mimi kuutumia muda huu kwa ajili yake na watoto wetu.” Aelezea kadamnasi. “Na pia  nawaomba radhi mashabiki zangu woote popote mlipo, kwa yaliyotokea. Nawashukuru pia kwa ushirikiano mkubwa na mapenzi ya dhati”
Inasemekana kuwa mapumziko hayo yatamnufaisha Celine pia ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya Uvimbe kwenye misuli ya koo
Hii ni mara ya pili kwa Rene kukabiliana na Cancer baada ya kwanza kutibiwa mwaka 1999, na Celine ameonesha hali chanya kuhusu kutibika kwa mumewe pindi alipohojiwa Julai Mwaka huu
 
Celine Dion akiwa na familia yake
“Maisha huamurisha baadhi ya vitu kwako, lakini anaendelea vizuri sana. Anafanya kazi kwa bidii, na amekuwa mtiifu sana, kitu ambacho si rahisi kwake. Hivyo, ni mtiifu, mchapakazi, anacheza na watoto na anafurahi pia” asema Celine.
Mwanadada huyo wa muziki wa taratibu alifunga ndoa na mwenzi wake mwaka 1994 baada ya kuonana kwa mara ya kwanza mwaka 1980. Kwa pamoja, wana watoto watatu wa kiume; Rene-Charles na mapacha wawili (Eddy na Nelson)

No comments: