Sunday, August 31, 2014

Gabrielle Union na Dwayne Wade wafunga ndoa kwa siri

Kama hukusikia kengele za Harusi na vigelegele duniani kote kwa siku ya jana, basi wewe si mjanja. Gabrielle Union na Dwayne Wade wameungana jana mjini Miami!
 
Sherehe hiyo ya wandani hao kati ya staa wa kike na muigizaji wa filamu mbalimbali nchini marekani, ambaye kwa sasa anaigiza pia kwenye Tamthilia ya “Being Mary Jane” (Gabrielle Union) amefunga ndoa na mcheza mpira wa kikapu wa timu ya Miami Heat hapo jana, iliyofanyika CHATEAU Artisan mansion.
Sherehe hiyo imefanywa kisiri kiasi cha kutokuwa wazi kwa vyombo vya habari, na inasemekana kuwa baadhi ya mastaa wa karibu na wanandoa hao kama John Legend, Essence Atkins na wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Miami Heat wamealikwa, kamailivyoripotiwa na gazeti la kila siku la nchini marekani.  
Wahusika wamekuwa wagumu kuachia picha za sherehe hiyo, lakini baadhi ya watu wamefanikiwa kupata picha zikiwaonesha wanandoa hao wakishereheka harusini.
Wandani hao walionekana kwenye mitandao ya kijamii siku moja kabla ya ndoa, wakionesha Hashtag #thewadeunion.

Na picha yake ikionesha wakiwa wanaondoka kutoka kwenye sherehe, yenye furaha ya maneno, “Lets goooooooo!” akimaanisha “Twende zetuuuuuuu” ikibeba tafsiri yao kuwa wapo zaidi ya tayari kwa fungate lao.
Picha ya Wade kwa mkewe pamoja na watoto wake, na binamu yenye maneno Kikosi


No comments: