Tuesday, October 7, 2014

Kelly Rowland asema ni "maajabu ya Mungu" kuwa mjamzito


Kelly Rowland asema ni "maajabu ya Mungu" kuwa mjamzito

PICHA zinazoendelea kuzagaa duniani zikimuonesha mwanadada Kerry Rowland akiwa mjamzito ndo hamasa kuu duniani kwa sasa.
Picha hizo zenye kuvutia, zimepigwa na Lane Gross kwa ajili ya jarida la Elle, kuhusu mahojiano aliyofanya na mwimbaji wa “Dirty Laundry” kuhusu namna anavyovutia akionekana kubeba kijacho.

Mwanamuziki huyo aliyetamba na kibao chake cha Motivation, Kelly, amesema kuwa ana hamu kubwa ya kuwa mama, na hawezi kusubiri kwa namna alivyojiandaa.
(Nimebakiza wiki chache tu, ninafurahi kumleta mtoto duniani, na kushiriki uzoefu huu, na mume wangu [Tim Witherspoon] hakika ni upande wangu wa pekee ninaoupenda”

Lance Gross/Elle via Instagram (@kellyrowland)

Akielezea vitu vizuri, Kelly (33) ametaja baadhi ya vyakula ambavyo amekuwa akila kipindi hiki cha ujauzito wake. “napenda Cherry Pie na Ice Cream ikichanganyika na Peanut butter.”


Instagram (@kellyrowland)

No comments: