Wednesday, February 18, 2015

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa kwenye Birthday ya FILAMONATA

Mambo yalikuwa mambo, yakinogeshwa na wageni lukuki kutoka kwenye tasnia ya Filamu nchini, wasanii, wanamuziki na waandaaji pia wa FILAMONATA na vipindi mwenza  walishiriki kuila keki hii tamu huku wakiburudishwa na dansi la uhakika.

utamu wa keki ulionjwa na kila aliyehusika kuisababisha FILAMONATA ifikie hapo ilipo, nikizungumzia watayarishaji, watangazaji na pia wawakilishi kwa niaba ya wasanii na wasikilizaji wetu.


kwa ufupi tuu, Sikiliza burudani ya pekee toka kwa DJ Charlie one, ambayo iliweza kusikika pia kwenye 100.5 Times FM radio katika kipindi cha Filamonata.
Kipindi pekee cha Filamu na wasanii kinachorushwa kila ya jumapili kuanzia saa tano kamili ya asubuhi mpaka saa saba ya mchana.
 

burudani hii ya kipekee iliambatana na shangwe za kusheherekea miaka mitatu ya kuanzishwa kwa FILAMONATA.
tulifurahije?

https://www.facebook.com/pages/Filamonata-Times-FM/357278257653209
Kuisikiliza, CLICK HERE

No comments: