Tuesday, December 1, 2015

Je, Unafahamu nini kuhusiana na Filamu ya NERIA (1993)?

Neria ni filamu ya kiafrika iliyotengenezwa nchini Zimbabwe mwaka 1993. Ni filamu pekee iliyojibebea umaarufu mkubwa sana barani Afrika na duniani kote kwa jinsi ilivyomnyanyua mwanamke wa kiafrika kuwa shupavu na kudai haki zake za msingi katika jamii.

       Filamu hii imetungwa na mtunzi mashuhuri wa nchini Zimbabwe, (Novelist) anayejulikana kwa jina la Tsitsi Ndangaremga, na kuandikwa Screenplay na Louise Riber; (ambaye pia ndiye mmoja wa waandaaji wa filamu ya Yellow Card (2000), Chumo (2011) na tamthilia ya Siri ya Mtungi (2012). Filamu ya Neria imeandaliwa (Produced) na John Riber akishirikiana na Louis Riber.
            Muongozaji wa filamu ya Neria ni Godwin Mawuru, ambaye amekuwa mwanasanaa maarufu mno nchini zimbabwe (katika kipindi cha uhai wake), akiwa kama muigizaji wa sanaaa ya jukwaani (theatre), Muongozaji (Director) na Mtayarishaji pia (Producer). Ndiye mtayarishaji wa tamthilia ya kwanza nchini humo ambayo ni ndefu na inayoendela kuoneshwa mpaka hii leo iitwayo STUDIO 263.
            Akiizungumzia filamu ya Neria kama alivyohojiwa na chombo kimoja cha habari cha nchini humo, kama filamu yake ya kwanza kuiongoza, amesema kuwa mchanganyiko wa muziki na Maigizo kwa pamoja unatia nguvu zaidi ya msisimko wa ujumbe husika, hasa ikizingatiwa kuwa wapokeaji si wapenda filamu pekee, bali pia Wanamuziki, huku ikigusa rika zote bila ya kubagua.
           
 Waigizaji waliopo kwenye filamu hiyo ni pamoja na Jesese Mungoshi – Neria. Ambaye pia ni  Muigizaji Maarufu sana wa kike nchini humo, aliyeolewa na Bwana Charles Mungoshi, Mwandishi nyota mwenye tuzo kedekede za uandishi. Kiufupi ni kwamba, Neria kaolewa kwenye familia ya Vipaji.

Waigizaji wengine ni pamoja na Dominic Kanavati – Phineas (amecheza filamu ya Mandela, 1987; Cry Freedom, 1987; Midday Sun, 1989; Emmanuel Mbrimi (Patrick) anthony Chinyanga (Mr. Chigwanzi); Violeth Ndlovu (Hmbuya); Claude Maredza – Mr. Machacha na wengineo.

            Nyimbo za filamu hii (Soundtrack) zimeimbwa na Muimbaji maarufu wa Afrika mwenye asili ya Kizimbabwe, anayejulikana kwa jina la Oliver Mtukudzi, a.k.a.Tuku

 
Filamu ya neria imekuwa filamu ya kwanza kinara nchini Zimbabwe kwa mauzo na pia moja ya filamu bora zenye mauzo mazuri barani Afrika kwa ujumla. Mauzo yake yanaendelea mpaka sasa kwani haichoki kutazamwa na rika zote, kizazi mpaka kizazi.
            Ni filamu inayoelezea mateso na mapambano ya haki za Mwanamke katika jamii ya kiafrika ambaye ameteseka kupata mirathi ya mali na malezi ya familia yake baada ya mumewe kufariki kwa ajali ya gari, kwenye kamji kadogo cha nchini Zimbabwe.

 Ajabu ni kwamba, utamu wa filamu hii unafahamika hadi nchini Marekani, ambapo imepata rate za 8.2 kwenye IMDB site. Imewahi kuandikwa na gazeti la Washington site, 4th Aprili 1993 kwenye ukurasa wa makala ikiwa na kichwa kikisema “Neria NR”, huku ikisifika kuwa ni filamu nzuri sana na bora iliyowahi kutengenezwa nchini Zimbabwe, ikitetea haki za wanawake kuhusiana na suala zima la mirathi.

No comments: