Friday, January 15, 2016

Washindani wa Oscar Academy Awards watajwa, Leonardo Di Caprio ang'araFilamu mpya kabisa iliyoigizwa na kinara Leonardo Di Caprio, “The Revenant,” simulizi  ya mtu jasiri anayelipiza kisasi, imekuwa kinara kwenye Ushindani wa tunzo za Oscar zilizotangazwa hapo jana, Nchini Marekani.
Filamu hiyo imepata nafasi 12 za kushindania tuzo za Oscar Academy, ikiwemo ile ya picha bora (Jongefu) ya mwaka, Muongozaji Bora, na Uchezaji bora wa Mastaa  Leonardo DiCaprio na Tom Hardy.
Ikifuatana kwa ukaribu zaidi na Filamu ya kisa cha Kupambania kuishi,  “Mad Max: Fury Road” imepata nafasi 10 za kuwania tuzo hizo za Utaalamu wa Filamu ikiwemo ya Filamu Bora, na Muongozaji Bora, mwenye uraia wa Australia aliyepumzika kwenye tasnia hiyo kwa miaka mitatu sasa kabla ya kuongoza filamu hiyo.
Jumla ya filamu nane zimechaguliwa kushiriki kuwania tuzo ya Filamu Bora ikiwemo  “Spotlight,” “The Martian,” “Bridge of Spies,”(007 James Bond)  “The Big Short,” “Room,” na kuhitimishwa na  “Brooklyn” .
Kwa mara nyingine tena, Wapigaji kura wa tuzo hizo wamepokea malalamiko kutoka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na muelekeo wao wa kuamua nani ashiriki tuzo hizo au laa, huku akikosekana muigizaji bora wa kiume mwenye asili ya kiafrika/mmarekani mweusi hata mmoja.
Malalamiko hayo kutoka kwa wadau wa filamu duniani ambayo yamekuwa yakisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Twittter dakika chache baada ya kutangazwa washindani hapo jana jioni, yamekuwa yakizihusisha filamu nzuri na zenye ubora wa pekee kama vile  “Concussion” (will smith) “Creed”( Michael B. Jordan), “Chi-raq” na “Beast of No Nation” (Idris Elba) zikikosa nafasi ya ushindani huku zikiwakilishwa na filamu pekee ya “Straight Outta Compton” yenye vijana wengi weusi, kwenye kundi la Original Screenplay pekee.
Malalamiko hayo yalidai uhalali huo kuwa ni mwaka wa pili sasa, tangu mwaka jana ambapo filamu stahiki iitwayo “Selma” ikiongozwa na Ava Du vernay iliyoigizwa na David Eyewolo kushindwa kushindana.  
Malalamiko hayo hayakuishia hapo, yalikwenda mbali zaidi nakudai kuwa Mafanikio ya Mauzo ya kihistoria  kwa filamu kinara, “Star Wars: The Force Awakens” imekosa nafasi kushiriki kwenye filamu bora ya mwaka, na badala yake kupata nafasi tano pekee kwenye ushindani wa kiufundi (technical categories)  hasahasa kwenye upande wa Sauti, Uhariri (Editing), na visual effects.
Filamu nyingine zilizotemwa kwenye kinyanganyiro cha  Best Picture ni “Straight Outta Compton,” stori maarufu ya kuanzishwa kwa kikundi cha muziki wa hip-hop; na “Creed” ambayo imeambulia nafasi moja ya Actor in a Supporting role (Sylvester Stallone) . Waongozaji waliotoswa (Directors ni pamoja na Steven Spielberg’s (“Bridge of Spies”),  Quentin Tarantino’s (“The Hateful Eight”), na Mwandishi wa Miswada  Aaron Sorkin (“Steve Jobs”)Alejandro Inarritu, aliyeshinda tuzo ya Muongozaji bora wa mwaka Jana kwenye filamu ya “Birdman” ameshiriki tena mwaka huu kwenye kazi yake mpya na inayotazamiwa zaidi iitwayo  “The Revenant.” Kwa miezi sasa, filamu hiyo imekuwa ikizungumziwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii namna matatizo yake ya kibajeti ya utengenezaji wa filamu hiyo yalivyoongezeka kutoka  $90 million to $135 million (Bilioni 180 mpaka Billioni 270) na kisha Dairekta huyo kuwasafirisha Cast na Jopo zima la waaandaaji mpaka kwenye kilele cha barafu kwenye milima midogo ya huko Argentina ndanindani, na uwanda wa wazi wa Canada, huku wakirekodi kwa mwanga asilia. (a.k.a. No taa)
Tuzo hizo zenye watazamaji ulimwenguni kote, zitaoneshwa live February 28, zikishehereshwa tena na Muigizaji mweusi, Chris Rock. Aliwahi kuwa MC mwaka 2005 na waandaaji wanaamini kuwa ataleta upekee, nguvu na mvuto wa ziada kwa watazamaji vijana waliokosa hamasa hiyo kwa miaka kadhaa. Mwaka jana, Neil Patrick Harris, alishika kipaza na watazamaji kushuka kutoka million 43 mpaka millioni 36.6 million.

Hii hapa ni list kamili ya washiriki wanaoshindania tuzo za mwaka  2016 za Oscars Academy:

Best motion picture of the year/Filamu bora (jongefu) ya mwaka:
“The Big Short”
“Bridge of Spies”
“Brooklyn”
“Mad Max: Fury Road”
“The Martian”
“The Revenant”
“Room”
“Spotlight”

Performance by an actor in a leading role/mwigizaji bora wa kiume(mhusika mkuu) wa mwaka:
Bryan Cranston in “Trumbo”
Matt Damon in “The Martian”
Leonardo DiCaprio in “The Revenant”
Michael Fassbender in “Steve Jobs”
Eddie Redmayne in “The Danish Girl”

Performance by an actress in a leading role/ muigizaji bora wa kike (mhusika mkuu) wa mwaka:
Cate Blanchett in “Carol”
Brie Larson in “Room”
Jennifer Lawrence in “Joy”
Charlotte Rampling in “45 Years”
Saoirse Ronan in “Brooklyn”

Performance by an actor in a supporting role/ Muigizaji bora wa kiume (uhisika msaidizi) wa mwaka:
Christian Bale in “The Big Short”
Tom Hardy in “The Revenant”
Mark Ruffalo in “Spotlight”
Mark Rylance in “Bridge of Spies”
Sylvester Stallone in “Creed”

Performance by an actress in a supporting role/ muigizaji bora wa kike (uhusika msaidizi) wa mwaka:
Jennifer Jason Leigh in “The Hateful Eight”
Rooney Mara in “Carol”
Rachel McAdams in “Spotlight”
Alicia Vikander in “The Danish Girl”
Kate Winslet in “Steve Jobs”

Achievement in directing/ Mafanikio kwenye Uongozaji :
“The Big Short” Adam McKay
“Mad Max: Fury Road” George Miller
“The Revenant” Alejandro G. Iñárritu
“Room” Lenny Abrahamson
“Spotlight” Tom McCarthy

Adapted screenplay (Filamu iliyotoholewa):
“The Big Short” Screenplay by Charles Randolph and Adam McKay
“Brooklyn” Screenplay by Nick Hornby
“Carol” Screenplay by Phyllis Nagy
“The Martian” Screenplay by Drew Goddard
“Room” Screenplay by Emma Donoghue

Original screenplay/Filamu halisia:
“Bridge of Spies” Written by Matt Charman and Ethan Coen & Joel Coen
“Ex Machina” Written by Alex Garland
“Inside Out” Screenplay by Pete Docter, Meg LeFauve, Josh Cooley; Original story by Pete Docter, Ronnie del Carmen
“Spotlight” Written by Josh Singer & Tom McCarthy
“Straight Outta Compton” Screenplay by Jonathan Herman and Andrea Berloff; Story by S. Leigh Savidge & Alan Wenkus and Andrea Berloff

Best animated feature film of the year/Katuni Bora (Ndefu) ya mwaka:
“Anomalisa” Charlie Kaufman, Duke Johnson and Rosa Tran
“Boy and the World” Alê Abreu
“Inside Out” Pete Docter and Jonas Rivera
“Shaun the Sheep Movie” Mark Burton and Richard Starzak
“When Marnie Was There” Hiromasa Yonebayashi and Yoshiaki Nishimura

Best documentary feature/ Makala Bora ya Mwaka:
“Amy” Asif Kapadia and James Gay-Rees
“Cartel Land” Matthew Heineman and Tom Yellin
“The Look of Silence” Joshua Oppenheimer and Signe Byrge Sørensen
“What Happened, Miss Simone?” Liz Garbus, Amy Hobby and Justin Wilkes
“Winter on Fire: Ukraine’s Fight for Freedom” Evgeny Afineevsky and Den Tolmor

Best foreign language film of the year/ Filamu bora ya lugha ya kigeni ya mwaka:
“Embrace of the Serpent” Colombia
“Mustang” France
“Son of Saul” Hungary
“Theeb” Jordan
“A War” Denmark

Achievement in cinematography/ Mafanikio katika Utaalamu wa kupiga picha (jongefu):
“Carol” Ed Lachman
“The Hateful Eight” Robert Richardson
“Mad Max: Fury Road” John Seale
“The Revenant” Emmanuel Lubezki
“Sicario” Roger Deakins

Achievement in costume design/ mafanikio katika Ubunifu wa Mavazi:
“Carol” Sandy Powell
“Cinderella” Sandy Powell
“The Danish Girl” Paco Delgado
“Mad Max: Fury Road” Jenny Beavan
“The Revenant” Jacqueline West

Best documentary short subject/ Makala(Fupi) Bora ya mwaka:
“Body Team 12” David Darg and Bryn Mooser
“Chau, beyond the Lines” Courtney Marsh and Jerry Franck
“Claude Lanzmann: Spectres of the Shoah” Adam Benzine
“A Girl in the River: The Price of Forgiveness” Sharmeen Obaid-Chinoy
“Last Day of Freedom” Dee Hibbert-Jones and Nomi Talisman

Achievement in film editing/ mafanikio katika Uhariri wa Filamu:
“The Big Short” Hank Corwin
“Mad Max: Fury Road” Margaret Sixel
“The Revenant” Stephen Mirrione
“Spotlight” Tom McArdle
“Star Wars: The Force Awakens” Maryann Brandon and Mary Jo Markey

Achievement in makeup and hairstyling/mafanikio kwenye Upambaji wa Nywele na Muonekano:
“Mad Max: Fury Road” Lesley Vanderwalt, Elka Wardega and Damian Martin
“The 100-Year-Old Man Who Climbed out the Window and Disappeared” Love Larson and Eva von Bahr
“The Revenant” Siân Grigg, Duncan Jarman and Robert Pandini

Achievement in music written for motion pictures (Original score)/ Mwandishi bora wa Muziki wa filamu (Mafanikio Asilia):
“Bridge of Spies” Thomas Newman
“Carol” Carter Burwell
“The Hateful Eight” Ennio Morricone
“Sicario” Jóhann Jóhannsson
“Star Wars: The Force Awakens” John Williams


Achievement in music written for motion pictures (Original song)/mwandishi bora wa muziki wa filamu (Nyimbo asilia):
“Earned It” from “Fifty Shades of Grey”
Music and Lyric by Abel Tesfaye, Ahmad Balshe, Jason Daheala Quenneville and Stephan Moccio
“Manta Ray” from “Racing Extinction”
Music by J. Ralph and Lyric by Antony Hegarty
“Simple Song #3” from “Youth”
Music and Lyric by David Lang
“Til It Happens To You” from “The Hunting Ground”
Music and Lyric by Diane Warren and Lady Gaga
“Writing’s On The Wall” from “Spectre”
Music and Lyric by Jimmy Napes and Sam Smith

Achievement in production design/ Mafanikio katika Ubunifu wa Uandaaji wa Filamu :
“Bridge of Spies” Production Design: Adam Stockhausen; Set Decoration: Rena DeAngelo and Bernhard Henrich
“The Danish Girl” Production Design: Eve Stewart; Set Decoration: Michael Standish
“Mad Max: Fury Road” Production Design: Colin Gibson; Set Decoration: Lisa Thompson
“The Martian” Production Design: Arthur Max; Set Decoration: Celia Bobak
“The Revenant” Production Design: Jack Fisk; Set Decoration: Hamish Purdy

Best animated short film/ Katuni Bora (Fupi) ya mwaka:
“Bear Story” Gabriel Osorio and Pato Escala
“Prologue” Richard Williams and Imogen Sutton
“Sanjay’s Super Team” Sanjay Patel and Nicole Grindle
“We Can’t Live without Cosmos” Konstantin Bronzit
“World of Tomorrow” Don Hertzfeldt

Best live action short film/Filamu bora (fupi) ya mwaka:
“Ave Maria” Basil Khalil and Eric Dupont
“Day One” Henry Hughes
“Everything Will Be Okay (Alles Wird Gut)” Patrick Vollrath
“Shok” Jamie Donoughue
“Stutterer” Benjamin Cleary and Serena Armitage

Achievement in sound editing/ Mafanikio katika Uhariri wa Sauti:
“Mad Max: Fury Road” Mark Mangini and David White
“The Martian” Oliver Tarney
“The Revenant” Martin Hernandez and Lon Bender
“Sicario” Alan Robert Murray
“Star Wars: The Force Awakens” Matthew Wood and David Acord

Achievement in sound mixing/ Mafanikio katika Uchanganyaji wa Sauti:
“Bridge of Spies” Andy Nelson, Gary Rydstrom and Drew Kunin
“Mad Max: Fury Road” Chris Jenkins, Gregg Rudloff and Ben Osmo
“The Martian” Paul Massey, Mark Taylor and Mac Ruth
“The Revenant” Jon Taylor, Frank A. Montaño, Randy Thom and Chris Duesterdiek
“Star Wars: The Force Awakens” Andy Nelson, Christopher Scarabosio and Stuart Wilson

Achievement in visual effects/ Mafanikio katika Kutengeneza Taswira zenye Matokeo :
“Ex Machina” Andrew Whitehurst, Paul Norris, Mark Ardington and Sara Bennett
“Mad Max: Fury Road” Andrew Jackson, Tom Wood, Dan Oliver and Andy Williams
“The Martian” Richard Stammers, Anders Langlands, Chris Lawrence and Steven Warner
“The Revenant” Rich McBride, Matthew Shumway, Jason Smith and Cameron Waldbauer
“Star Wars: The Force Awakens” Roger Guyett, Patrick Tubach, Neal Scanlan and Chris Corbould
Chanzo Variety

No comments: