Saturday, March 11, 2017

Tanzania Yangu, Nchi Yangu

nimekuwa nikiwaza kwa muda mrefu pasipo kuwa na jibu. huenda sina kipaji kikubwa cha kuifanya nchi yangu ifaidi kupitia mimi, ila sitoshindwa kufanya chochote kwa ajili ya nchi yangu. kwa hilo ninaamini sana.

nilipokuwa kijana, rafiki zangu weengi waliwahi kuniambia kuwa nina 'hood' ya kimarekani zaidi, au wakisema kuwa mi ni wa mbele, sikupaswa kuzaliwa hapa Bongo. nililewa sifa na kuwa bishoo kupindukia, nikiona raha kwa maneno yao ya ajabuajabu. mpaka nilipopata ufahamu kuwa ninapoteza muda pasipo kufanya mambo ya msingi na maana kwa ajili ya nchi yangu, na hata mimi mwenyewe.

wazo la kutengeneza hivi limetokana na umuhimu wa kuuonesha upendo wa nchi yangu. Nimekuwa msemaji wa maneno mengi, nikitoa maoni mbalimbali na hata kushabikia vitu vingi visivyo asili yangu, huku nikisahau mambo meengi mazuri ambayo yapo nchini kwangu pekee, na hayapo hata chembe sehemu nyinginezo hapa duniani.

na hii ni kasumba ya vijana wengi hapa nchini, ambao hupenda kusifia au kupendelea vya wageni na kuvikataa vya kwao. kwa wataalamu wa mambo ya falsafa na sayansi ya Jamii (Sociology) huipa jina dhana hiyo la Xenocentric Culture.

utampendaje 50 cent, kendrick Lamar au Joe cole huku ukimuacha Joh Makini, Ali Kibba na Diamond kama wanamuziki wako? utaachaje bendi safi za muziki wa asili ya tanzania, au hata za dansi safi la msondo na sikinde na kwenda kutukuza muziki wa kikongo na wa magharibi?

utumwa wa fikra. utumwa mabao ukiuendekeza, unakuwa masikini. Ni heri uwe masikini kifedha kuliko kifikra. unashindwaje kuzitambua mbuga za wanyama tele zilizopo hapa nchini? Mbuga ya kwanza duniani yenye tawala yake mpaka baharini? nyumbani kwa flamingo, sokwe wa ajabu na pekee huko songwe, vyura wa kihansi, Mlima mrefu barani afrika na maajabu yake, na mengineyo meengimeengi mengi.

jiji linalokua kwa kasi barani afrika, lipo Tanzania. tuna kila kitu kizuri, ila tunashindwaje kuvitukuza?

jaribu kutizama hii video fupi, alafu ujionee mazuri yaliyopo nchini kwetu

No comments: