Na DJ Charlie One
Msanii mwanamuziki na muigizaji anayekimbiza vilivyo kwenye chati za
muziki nchini marekani, Selena Gomez amekuwa akitoka na kuachana na Justin Bieber tangu
mwaka 2010, ambapo mara yao ya mwisho kuachana ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu.
akizungumza na chombo kimojawapo cha habari, rafiki wa karibu na wa kuaminika wa mwanamuziki selena Gomez amedai kuwa kuachana huko kati ya Justin na Selena
kumeonekana kuwa na kheri ndani yake.
“anataka kusonga mbele kutoka kwenye matatizo ya
kimahusiano” rafiki wa karibu aeleza
Ingawa mwanamuziki Selena pamoja na Justin Bieber
wameonekana wakiwa pamoja kwa miezi ya karibuni, rafiki huyo wa karibu amedai
kuwa haitotokea tena.
“hajarudiana naye, anajua kuwa si salama, lakini si
rahisi kumuacha mazima” chanzo hicho kiliongezea
Kumsaidia kupunguza msongo wa mawazo, mnamo mwezi
uliopita mwanamuziki Selena Gomez alikwea pipa mpaka Ufaransa na Cara Delevigne
kuisheherekea kumbukumbu yake ya 22 ya kuzaliwa (Birthday)
Ni vizuri kwa yeye kwenda mbali na kufurahi” rafiki
huyo wa karibu aongezea.
Selena kwa sasa anatilia mkazo zaidi fursa zake za kuigiza.
Filamu ya Muziki, Rudderless inayotarajiwa
kuonekana kwenye sinema mnamo mwezi Oktoba
Chanzo: music-news.com
No comments:
Post a Comment