Kelly Rowland asema ni "maajabu ya Mungu" kuwa mjamzito
PICHA
zinazoendelea kuzagaa duniani zikimuonesha mwanadada Kerry Rowland akiwa
mjamzito ndo hamasa kuu duniani kwa sasa.
Picha hizo
zenye kuvutia, zimepigwa na Lane Gross kwa ajili ya jarida la Elle, kuhusu
mahojiano aliyofanya na mwimbaji wa “Dirty Laundry” kuhusu
namna anavyovutia akionekana kubeba kijacho.
Mwanamuziki
huyo aliyetamba na kibao chake cha Motivation, Kelly, amesema kuwa ana hamu
kubwa ya kuwa mama, na hawezi kusubiri kwa namna alivyojiandaa.
(Nimebakiza
wiki chache tu, ninafurahi kumleta mtoto duniani, na kushiriki uzoefu huu, na
mume wangu [Tim Witherspoon] hakika ni upande wangu wa pekee ninaoupenda”
Lance Gross/Elle via Instagram (@kellyrowland)
Akielezea vitu
vizuri, Kelly (33) ametaja baadhi ya vyakula ambavyo amekuwa akila kipindi hiki
cha ujauzito wake. “napenda Cherry Pie na Ice Cream ikichanganyika na Peanut
butter.”
Instagram (@kellyrowland)
No comments:
Post a Comment