Friday, May 1, 2015

Monalisa azungumza na Mashabiki wake kwa namna ya kipekee


Msanii wa filamu nchini tanzania anayejulikana kwa jina la Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa amevunja ukimya kwa kuibuka upya na kuzungumza na mashabiki wake kwa namna ya kipekee.

akiongea katika video fupi aliyorekodiwa na kampuni ya Cherrie Company, amewaondoa hofu mashabiki wake ambao wamekuwa na kiu ya kutomuona mara nyingi katika luninga kuliko wanavyoonekana wasanii wengine.

"watu wengi wamekuwa wakiniulizia kuwa mbona kimya, nimepotea, au nimeacha kuigiza, ila kiukweli nipo na ninaendelea kuigiza kama kawaida na nitaendelea kuwa nanyi mashabiki zangu" alisisitiza Yvonne (Monalisa).


katika video hiyo, ameonekana pia akiwaonesha tuzo za mafanikio ya uigizaji mashabiki zake wa timu monalisa kwa kuwathibitishia kuwa ni namna gani yeye alivyo bora, kwa kadiri Mashabiki wake wanavyozidi kumpa bidii ya kufanya kazi nzuri.

"Kiukweli nawaheshimu sana mashabiki zangu, kwani wamekuwa na mimi tangu naanza sanaa hii ya uigizaji tangu mwishoni mwa miaka ya tisini mpaka sasa. ni zaidi ya miaka kumi na sita sasa, na tumekuwa familia kubwa inayozidi kukua na kuongezeka kila siku"

akizungumza na mwandishi wetu, kwa upande wake, Yvonne (Monalisa) ameizungumzia video hiyo fupi kama njia maalum aliyoamua kujiwekea ili kuzungumza na mashabiki wake kuhusiana na kazi anazozifanya.


Mmoja wa Mashabiki wa Yvonne Cherrie (Monalisa), Vaileth Kilawe, amemuelewa sana monalisa kwa jinsi anavyojali Mashabiki wake kuanzia kwenye mitandao ya kijamii, na hata wale wasio katika teknolojia hiyo.

"Nampenda sana Mona coz sijamsikia katika skendo yoyote, na pia napenda sana anavyojua kuitunza ngozi yake" alisema Vaileth.

Kwa sasa, Yvonne Cherrie ni mmoja wa majaji wa Tanzania Movie Talent (TMT), na ameingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya Muigizaji bora wa kike kutoka kwenye tuzo mpya za filamu nchini maarufu kama Tanzania Film Awards (TAFA) zitakazofanyika mwezi huu

No comments: