Wednesday, August 13, 2014

Selena Gomez kwa sasa inamuwia vigumu kuachana kabisa na Justin Bieber


Na DJ Charlie One

Msanii mwanamuziki na muigizaji anayekimbiza vilivyo kwenye chati za muziki nchini marekani, Selena Gomez amekuwa akitoka na kuachana na Justin Bieber tangu mwaka 2010, ambapo mara yao ya mwisho kuachana ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu. 


akizungumza na chombo kimojawapo cha habari, rafiki wa karibu na wa kuaminika wa mwanamuziki selena Gomez amedai kuwa kuachana huko kati ya Justin na Selena kumeonekana kuwa na kheri ndani yake.
“anataka kusonga mbele kutoka kwenye matatizo ya kimahusiano” rafiki wa karibu aeleza
Ingawa mwanamuziki Selena pamoja na Justin Bieber wameonekana wakiwa pamoja kwa miezi ya karibuni, rafiki huyo wa karibu amedai kuwa haitotokea tena.


“hajarudiana naye, anajua kuwa si salama, lakini si rahisi kumuacha mazima” chanzo hicho kiliongezea

Kumsaidia kupunguza msongo wa mawazo, mnamo mwezi uliopita mwanamuziki Selena Gomez alikwea pipa mpaka Ufaransa na Cara Delevigne kuisheherekea kumbukumbu yake ya 22 ya kuzaliwa (Birthday)

Ni vizuri kwa yeye kwenda mbali na kufurahi” rafiki huyo wa karibu aongezea. 

Selena kwa sasa anatilia mkazo zaidi fursa zake za kuigiza. Filamu ya Muziki, Rudderless inayotarajiwa kuonekana kwenye sinema mnamo mwezi Oktoba

Chanzo: music-news.com

No comments: