Thursday, June 21, 2018

NGUVU YA SOCIALIZATION KATIKA BIASHARA YAKO

Karibu Nikuhudumie.

ushawahi kujiuliza kwanini biashara za watu waliokuwa serious na Network Marketing zinakua haraka sana na kufanikiwa kwa urahisi kuliko direct marketing?
well, suluhu yake ni rahisi zaidi. Socialization. Yes, SOCIALIZATION!!!
kila kazi ya mikono unayoifanya pasipo socialization ni kazi bure. kama unafikiria kujiajiri,ni lazima ujenge SOCIALIZATION kama unataka kuata zaidi. ila kama unataka kupata kidogo, sio mbaya ukiwa na uelewa mbaya sana wa socialization, lakini, ni lazima utakuwa nao hata kiduuchu.
jaribu tuu kujiuliza, socialization ni nini? kwanini kuna SOCIAL MEDIA? Je, imetokana na SOCIALIZATION? inafanyeje kazi kwenye kukua na kundelea kwa biashara yangu?

historia ya socialization ilianza tangu mwanadamu wa kwanza alipoanza kutengeneza jamii na makazi ya kudumu, mnamo miaka milioni 750 iliyopita. huu ni wakati ambao mwanadamu wa kwanza alianza kugundua talanta nyingine mbalimbali za kumfanya aishi, mfano uvuvi, ukulima, kuchonga vyuma na kadhalika. maana hapa aliachana na kutegemea mawindo pekee.

dunia ya sasa tuna maendeleo makubwa sana ya sayansi na teknolojia ambayo yanatupeleka kwenye zama za kale tena pasipo kujielewa. mf. unaweza kula,kuoga, kuvaa na kununua chochote ukiwa chumbani mwako. ukiwa na simu ya mkononi, mtandao (network) na kifaa cha internet (Simu,iPad, Laptop, etc) vinatosha kununua chochote hata kama ni umeme,chakula, maji, nk. na ukaletewa mpaka chumbani mwako. je, unapataje muda wa kuSOCIALIZE na wenzio?

suala linakuja pale unapokuwa na uhitaji wa fedha au kukua kwa biashara yako. unahitaji uwe star wa ghaflagafla ili uuze na kufanya bashara vizuri. unauzaje sasa? SOCIALIZATION.

1. JUA UNAUZA NINI KWA WATEJA WAKO.
     hata kama unauza bidhaa ya aina yoyote ile, ni vyema ukafunua kichwa chako na kufikiria kwa undani ili kujua bidhaa yako ni nini na ina malengo gani kwa mtumiaji. hapa naomba nieleweke vizuri. suala sio kujua biashara yako kwa jina tuu, maana utakuwa wa ajabu kama hujui vyema jina la biashara yako; bali namaanisha kujua vizuri kile unachokiuza. hembu nikutolee mfano. unataka kufanya biashara ya ndizi, ila hujui hata ni ndizi za aina gani zilizopo duniani, na sokoni, zipi zina faida/hasara, utunzaji wake, zinakomaaje, mbivu zikoje na mbichi zinakuwaje.

angalizo la kujua biashara yako ni la muhimu kulikomambo yote, hata kama baishara yako hauijui vizuri. maana, kama haujui bidhaa unayouza, ni sawa na kutojua kinachoendelea katika biashara yako.

2. JUA UNAUZA WAPI BIASHARA YAKO
      heheh, eti kuna watu huwa wanauza mchicha jeshini, au wanauza samaki ziwani. hatusemi kama unaweza usiuze, la hasha, ila unaweza ukauza kwa hasara au ukapiga nayo picha biashara yako. utafiti mwepesi unaanzia pale unapoishi, na maeneo ya jirani. maeneo yenye msongamano wa watu wengi yanaweza kuwa na nafasi nzuri kwa wewe kufanya biashara, laikin pia yanategemea na uhitaji wa bidhaa hiyo na asili yake. kwa mfano. kwenye kituo cha basi, kuna wasafiri, maana bidhaa zinazoendana na usafiri zitafanya kazi.

Stendi ya Mabasi Mkoani unaweza kufanya biashara ya vitu vya kula wasafiri, pipi, chocolate, juices na mikate. ila pia uanweza kuuza, ukifikiria kwa undani; bidhaa maalum pasipo kutegemea. mf. watu wanaoishi Kanda ya ziwa hununua sana mafuta ya alizeti wakiika singida. kanda ya ziwa nazi moja huuzwa kwa tshs.1600/= hadi tshs. 2000/= lakini je, unaowauzia bidhaa yako wana uelewa na hamu nayo hiyo bidhaa?

3. UNAMUUZIA NANI BIASHARA YAKO.
 SOCIALIZATION inakupa jibu la jambo hili. unapokutana na watu wengi zaidi, unajifunza mengi zaidi. wataalamu wa biashara ya mtandaoni wanaweza kunithibitishia hili. unajuana na watu kumi, wale kumi wakiongea na wengine kumi, nao pia wakawaambia na wengine, wanakuwa watu zaidi ya thelatini. sasa fikiria kama unajuana na watu mia..unajua???
well, hizo story zipo sana vichwani vyao. ila ujanja halisi ni huu. unawasiliana vipi na watu kwenye kujichanganya nao na wakajua wewe unafanya nini hapa duniani? hilo ndilo la msingi. aidha wakucheke, wakununie, wakuponde, au wakusilibie. huenda usijali sana. maana wakikuita yule fundi kimeo, ujue wameuona ufundi wako, ingawa ni kimeo, ila siku wakimhitaji fundi ni lazima wakukumbuke.

4. UNAUZA NINI KWA WATEJA WAKO
Huenda ukachelewa kupata kazi na kuitwa kutoa huduma kama upo  eneo lenye ushindani mkubwa, ila ni muhimu mtu akujue tuu kila anapokuona, au anapoiona bidhaa yako. mteja ajue unauza nini. mfano unauza bidhaa za chooni,lazima ziwe na muonekano wa chooni. chookinatakiwa kiwe kisafi muda wote, hivyo kama unauza dawa ya chooni, ni muhimu kuiweka kwenye mahala pasafi na enye kuvutia usafi, ili ile imani ya bidhaa yako kufanya kazi kwa ufanisi iwepo. sio unauza dawa ya chooni, alafu dawa yenyewe ipo kama choo. kaah! atanunua nani?

5. UNA MUONEKANO GANI KWA WATEJA WAKO WAPYA?
     amini kuwa, kila mteja ni mpya,hasa kama umeuona ushindani wa hatari kwenye dunia yetu ya sasa isiyo na kitu kipya. kila unachofikiria yupo mwenzio aliyefikiria kabla yako na akafanya. sasa yanini kujiona wewe ni bora kuliko mwenzio? au labda useme kuwa unamringishia..
wengine hujali sana SOCIALIZATION interraction hasa wakiona wateja wapya. hubadilishana nao mawasiliano na kuonesha namna wanavyojali biashara yao, na thamani ya kutoa huduma bora zaidi. Vitu kama Business Cards na Flyers hutolewa kwa ukarimu na huduma bora ya kumsikiliza mteja angalau tuu akufikirie wewe kwanza kwenye biashara yako. wel, they work! Trust Me!

SOCIALIZATION NI NINI?
Socialization ni kujichanganya. Kuwa Makini, Kujitambua, Kuchanua Biashara, Kupangilia Mikakati yako, Kugawanya Majukumu ya Biashara yako. KUJICHANGANYA. ukiwa makini utanielewa vizuri. maana vyote nimevitaja hapo Juu.

DJ Charlie One.
Charlieonetz  June, 2018.

No comments: